Home / NEWS / Rais Pierre Nkurunziza afanya ziara nje ya nchi kwa mara ya kwanza tangu 2015

Rais Pierre Nkurunziza afanya ziara nje ya nchi kwa mara ya kwanza tangu 2015

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameondoka nchini mwake kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka miwili, tangu kutofanikiwa katika  jaribio la kumwondoa madarakani mwaka 2015.

Nkurunziza amezuru nchini Tanzania katika Wilaya ya Ngara, kukutana na mwenyeji wake rais John Magufuli.

Ziara hii imekuja wakati huu Tanzania ikiendelea kutoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 200,000 waliokimbia nchi yao kwa sababu za kiusalama.

Rais Nkurunziza ameandamana na idadi kubwa ya Mawaziri wake katika ziara hiyo ya kwanza ambayo ilitangazwa katika dakika za lala salama.

Jaribio la kumpindua Nkurunziza lilifanyika wakati akihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiwahotubia wananchi, rais Nkurunziza amewaambia wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania kurejea nyumbani ili kuijenga nchi yao.

“Tunawaomba raia wa Burundi wanaoishi hapa nchini Tanzania, kurudi nyumbani ili tuijenge nchi yetu,” alisema.

Aidha, ameishukuru Tanzania kwa kuwa jirani mwema na kuwapa hifadhi raia wa Burundi waliokimbia nchi yao.

Rais Magufuli amesisitiza ujumbe wa rais Nkurunziza na kuwataka wakimbizi hao kuchukua hatua za kurudi nyumbani kwa hiari.

“Rudini nyumbani kwa hiari, sisi hatutawafukuza,” alisema rais Magufuli.

Mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kutoweka kwa mujibu wa Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za Binadamu kama Human Rights Watch.

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa ni mratibu wa mazugumzo ya kisiasa nchini humo, ambaye ameendelea kujaribu kuwaleta wapinzani wa kisiasa nchini humo kujaribu kuleta mwafaka wa kisiasa nchini humo.

Hata hivyo, kumekuwa na changamoto ya kuwakutanisha wanasiasa wa upinzani na viongozi wa serikali.   >>>   CHANZO CHA HABARI <<

380 total views, 1 views today

About Steven Blaiton

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

x

Check Also

AFRIKA KUSINI : Wanawake ‘wacheza utupu’ watumbuiza wafungwa Afrika Kusini

Picha za wanawake hao wakiwaburudisha wafungwa zilianza kusambaa mitandao ya kijamii Wafungwa ...

Copy Protected by Chetan's WP-Copyprotect.

Powered by themekiller.com anime4online.com animextoon.com apk4phone.com tengag.com moviekillers.com