Home / NEWS / FAO: Samaki aina ya sato au Tilapia apatikana na virusi katika baadhi ya nchi

FAO: Samaki aina ya sato au Tilapia apatikana na virusi katika baadhi ya nchi

 • Samaki aina ya sato au Tilapia apatikana na virusi katika baadhi ya nchi 

  Maradhi hatari yanayoambukiza yanasambaa miongoni mwa samaki aina ya sato au tilapia, moja ya samaki muhimu na mashuhuri kwa matumizi ya binadamu.

  Tahadhari hiyo imetolewa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO likisema mlipuko wa maradhi hayo uchukuliwe kwa tahadhari na nchi zinazosafirisha sato zihakikishe zimechukua hatua madhubuti za kudhibiti hatari ya virusi hivyo kwa kuimarisha upimaji, kusisitiza hati za afya, kuchukua hatua za kuarantini na kujiweka tayari na mipango ya dharura.

  Kwa mujibu wa kitengo cha FAO cha habari na mfumo wa tahadhari ya mapema kilichotoa tangazo hilo, virusi hivyo vinavyoitwa Tilapia Lake Virus (TiLV) sasa vimeshathibitishwa katika nchi nne kwenye mabara matatu duniani ambazo ni Colombia, Ecuador, Misri na Thailand na pia katika utawala wa Israel.

  Mchuzi wa Sato na Sima

  FAO inasema ingawa kwa sasa virusi hivyo havina hatari yoyote kwa afya ya binadamu, kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri usalama wa chakula na lishe duniani. Mwaka 2015 biashara ya sato duniani ilikadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 1.8.

  China, Indonesia na Egypt ni nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa sato, samaki ambaye pia utumizi wake unazidi kuimarika katika nchi za Afrika

  >CHANZO  CHA HABARI  HAPA<

1,173 total views, 2 views today

About Steven Blaiton

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

x

Check Also

Ufaransa yachangia Euro 250,000 kusaidia wakimbizi Tanzania

Msaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumi Serikali ya Ufaransa imechangia ...

Copy Protected by Chetan's WP-Copyprotect.

Powered by themekiller.com anime4online.com animextoon.com apk4phone.com tengag.com moviekillers.com