Home / NEWS / BURUNDI: Serikali ya Burundi imetangaza kuwa watu 700 wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa malaria

BURUNDI: Serikali ya Burundi imetangaza kuwa watu 700 wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa malaria

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa watu 700 wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miezi miwili iliyopita nchini humo.

Mabadiliko ya tabianchi na umasikini wa kupindukia unaowakabili watu wengi wa nchi hiyo vimetajwa kuwa sababu ya vifo hivyo.

Waziri wa Afya nchini Burundi, Dakta Josiane Nijimbere amesema tangu Januari Mosi hadi Machi 10 mwaka huu, watu zaidi ya milioni moja na laki nane wameambukizwa malaria, ambapo 700 miongoni mwao wamepoteza maisha, sawa na takriban watu 10 kila siku.

Waziri wa Afya nchini Burundi, Dakta Josiane Nijimbere

Serikali ya Burundi imesema inahitaji dola milioni 31 za Marekani ili kukabiliana na maambukizi mapya ya malaria, mripuko unaotokea wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa.

Maginwja ya kipindupindu na malaria yameenea sana kipindi hiki katika nchi za Afrika. Oktoba mwaka jana, watu karibu 50 waliaga dunia ndani ya siku 30 katika jimbo la Sokoto, kaskazini magharibi mwa Nigeria kutokana na malaria.

Mwaka jana Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria utaangamizwa kabisa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa sana na maradhi hayo ifikapo mwaka 2020.

20,116 total views, 1 views today

About Steven Blaiton

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

x

Check Also

Ufaransa yachangia Euro 250,000 kusaidia wakimbizi Tanzania

Msaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumi Serikali ya Ufaransa imechangia ...

Copy Protected by Chetan's WP-Copyprotect.

Powered by themekiller.com anime4online.com animextoon.com apk4phone.com tengag.com moviekillers.com